Akifafanua suala hilo Rashid Falih, kamanda anayesimamia masuala ya usalama katika mji wa Samarra amesema kwamba kikosi maalumu tayari kimetayarishwa na kupewa mafunzo ya dharura kwa ajili ya kushughulikia suala la usalama katika mji huo wakati wa kufanyika maombolezo hayo. Amesema kuwa Wizara za Ulinzi na Mambo ya Ndani za Iraq zinashirikiana vyema na kikosi hicho kwa ajili ya kudhamini usalama wa mji huo wakati wa kufanyika maombolezo yaliyotajwa.
Kamanda Rashid Falih amesema kuna mipango maalumu ya kutumiwa vikosi vya askari usalama kutoka mji mkuu Baghadad ili kulinda usalama katika maeoneo tofauti ya kuingia na kutoka mjini huo. Amesema licha ya masuala ya kiusalama kuna mipango mingine muhimu ya kutoa huduma tofauti zikiwemo za tiba na chakula kwa waombolezaji watakaozuru mji huo.
Tarehe Mosi Februari sawa na tarehe 8 Rabiul Awwal 1433 Hijiria ni siku ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi Imam Hassan Askari (as) ambaye ni Imam wa 11 wa wafuasi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw). 942063