Awali Sheikh Muhammad as-Salami, mkuu wa taasisi iliyotajwa alitangaza kuwa taasisi hiyo ina lengo la kuanzisha ofisi zake za uwakilishi katika mji wa Arbil pamoja na mikoa mingine ya katikati na kusini mwa nchi hiyo.
Amesema taasisi hiyo pia imewasilisha ombi la kutambuliwa rasmi na Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Kielimu ya Iraq.
Wakuu wa Taasisi ya Qur'ani Tukufu pia wamewasilisha ombi la kutaka kunufaika na maustadhi mashuhuri wa Qur'ani wa Misri wakiwemo Muhammad Khalifa, Ahmad Ahmad Nuina' na Farajullah as-Shadhili kwa kuitaka iruhusu maustadhi hao waitembelee Iraq kwa lengo la kunyanyua kiwango cha kiraa na usomaji Qur'ani nchini humo.
Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya Haram ya Hadhrat Abbas (as) hujishughulisha na masuala ya kuinua kiwango cha utamaduni wa Qur'ani na usomaji sahihi wa kitabu hicho kitakatifu nchini Iraq. 943477