Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA barani Ulaya, kongamano hilo litajadili nafasi ya vituo vya elimu vya Kiislamu ambavyo vimechangia katika elimu karne zilizopita na mabadiliko katika zama hizi.
Vituo vya kale vya Kiislamu vya elimu kama vile Al Azhar vimewavutia wanafunzi ambao baada ya kuhitimu hapo hueneza elimu walikotoka.
Kongamano hilo litachunguza vituo vitatu vya elimu ambavyo vina nafasi muhimu katika kueneza fikra katika jamii za Waislamu.
Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Cairo, Misri, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Madina, Saudi Arabia na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa cha Qom, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kongamano hilo litachunguza stratijia za vyuo hivyo katika kueneza elimu kote duniani pamoja na hatua zilizochukuliwa na waliohitimu katika kutekeleza waliyojifunza katika jamii zao.
943539