IQNA

Taxi za Waislamu zazinduliwa Ujerumani

13:26 - January 31, 2012
Habari ID: 2265273
Muislamu mmoja huko Ujerumani ameanzisha tovuti ya huduma ya taxi za Waislamu ambapo Wajerumani wanaweza kusafiria katika magari ya jinsia moja, tovuti ya thelocal.de imeripoti.
'Wanawake na Wanaume Waislamu wamelalamika kwa wingi kuwa hawawezi kutumia mfumo wa kawaida wa usafiri kwa sababu sheria za Kiislamu za kutenganisha jinsia hazitekelezwi,' Selim Reid mwenye umri wa miaka 24 kutoka mji wa Norderstedt karibu na Hamburg ameliambia gazeti la Hamburger Abendblatt.
Fikra ya tovuti ya muslimtaxi.de ilianziswa kwanza na Reid baada ya masaibu waliyoyapata wazazi wake.
Amesema alipata motisha wa kuanzisha tovuti hiyo baada ya wazazi wake, ambao wana asili ya Iraq, kupanda taxi ambayo dereva wake aliyekuwa na chuki dhidi ya Waislamu walitumia muda wote kuwakosoa.
'Dereva huyo na watu waliokuwa ndani ya taxi walionyesha chuki kubwa dhidi ya wageni na hasa hijabu ya mama yangu' Reid ameliambia gazeti hilo.
'Dereva huyo alidhani wazazi wangu hawafahamu Kijerumani,' ameongeza.
Tovuti hiyo iliyoanzishwa mwishoni mwa mwaka 2011 inawaruhusu Wajerumani wanaojali maadili kutumia taxi ambazo suala la kutenganisha jinsia linazingatiwa. Reid amesema tayari maelfu ya watu wamefurahishwa na huduma za taxi ya Waislamu.
'Kutenganisha jinsia ni sehemu ya imani yetu na Uislamu ni sehemu ya Ujerumani,' amesema Reid.
Kuna karibu Waislamu milioni 4.3 Ujerumani ambao ni asilimia 5 ya watu milioni 83 nchini humo.
943451
captcha