IQNA

Kongamano la Mapinduzi ya Tunisia katika Mtazamo wa Sira ya Mtume kufanyika Qairawan

20:14 - February 01, 2012
Habari ID: 2266849
Kongamano la Mapinduzi ya Tunisia katika Mtazamo wa Sira ya Mtume (saw) limepangwa kuanza kesho tarehe 2 hadi 3 Februari katika mji wa Qairawan nchini Tunisia.
Kongamano hilo la kitaifa litahudhuriwa na maulamaa wa Kiislamu, wanafikra, wahakiki na wahadhiri wa vyuo vikuu na lengo lake ni kuchunguza sura ya kidini ya mapinduzi ya wananchi wa Tunisia na jinsi yalivyooana na sheria na maamrisho ya Mtume Muhammad (saw).
Washiriki katika kongamano hilo watajadili maudhui kama matokeo ya mapinduzi ya Tunisia, mapinduzi na kujikomboa katika makucha ya dhulma katika sira ya Mtume (saw), mapambano dhidi ya tawala za kidikteta katika mtazamo wa mafundisho ya Kiislamu, kueneza Uislamu bila ya kuzusha hitilafu katika umma, mapatano ya kitaifa na uadilifu baada ya mapinduzi.
Sherehe za ufunguzi wa kongamano hilo la kitaifa itahudhuriwa na Spika wa Bunge la Waasisi Mustapha Ben Jaafar na Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Tunisia Nouruddin al Khadimi. Kongamano hilo litafungwa na Rais Moncef Marzouki.



captcha