Tovuti ya Columbiamsa imeripoti kuwa, semina hiyo ni sehemu ya mpango wa Wiki ya Ujue Uislamu inayofanywa kwa hima ya Jumuiya ya Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Columbia kuanzia tarehe 9 hadi 19 Februari.
Semina hiyo itachunguza sauti, lahani, mbinu za kijadi za kiraa ya Qur'ani na sifa makhsusi za kilugha za Qur'ani. Vilevile itachunguza ujumbe mkubwa ulioko kwenye kisa cha Nabii Mussa (as) ndani ya kitabu cha Qur'ani Tukufu.
Ratiba nyingine za semina hiyo ni pamoja na 'rangi za Kiislamu', 'sira ya Mtume (saw)', 'jirani Muislamu' na 'swala ya Ijumaa.
Wiki ya Ujue Uislamu inafanyika kwa shabaha ya kuwaelimisha wanachuo na wananchi wa Marekani na kuondoa taswira mbaya iliyoenezwa katika jamii kuhusu dini hiyo tukufu. 945333