IQNA

Taasisi ya Al Mahdi yaanzishwa Afghanistan

14:35 - February 04, 2012
Habari ID: 2267749
Waislamu nchini Afghansitan wameanzisha Taasisi ya Al Mahdi (ATF) kwa lengo la kueneza mafundisho ya Kiislamu, utamaduni wa kidini na kuandaa mazingira ya Umoja wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Kabul, Taasisi ya Al Mahdi ilianzishwa juzi katika mji wa Kondoz Kaskazini mwa Afghanistan katika sherehe ambazo zilihudhuriwa na maafisa wa serikali, viongozi wa kieneo, wanazuoni wa kidini, wanachuo wa kidini, walimu na wanafunzi.
Mbali na programu maalumu za kiutamaduni, kijamii na kidini, taasisi hii pia itaandaa programu kuhusu masuala ya kila siku.
Taasisi ya Al Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) ina kituo cha utamaduni, maktaba ya umma maalumu kwa wanazuoni, vijana na wanafunzi wanaotafuta vitabu vya kisayansi na kielimu.
Taasisi hii pia itachapisha jarida la kila wiki litakalojulikana kwa jina la Al Mahdi ambalo litachambua masuala ya kiuchumi, kielimu, kijamii na kimaadili.
946081
captcha