Kikao cha pili cha Mwamko wa Kiislamu, Mwangwi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kinafanyika leo Jumatatu katika Husainiya ya al Zahra (as) ya Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu mjini Tehran.
Kikao hicho kinasimamiwa na Kituo cha Mapambano cha Basij na Kituo cha Kutarjumu na Kueneza Maarifa ya Kiislamu na Sayansi za Jamii.
Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu Muhammad Reza Dehshiri amefungua kikao hicho kwa kuzungumzia taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika mwamko wa sasa wa Kiislamu.
Wazungumzaji wengine katika kikao hicho wanajadili maudhui ya nara na kaulimbiu za mwamko wa sasa wa Kiislamu na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 948167