Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo linafanyika kwa ushirikiano baina ya Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti na Kituo cha Utafiti na Elimu ya Kijamii katika Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia Iran.
Sayyid Abdul Amir Nabavi afisa wa habari katika Kituo cha Utafiti na Elimu ya Kijamii amesema makala zilizofupishwa 306 na makala kamili 149 kutoka Iran na nchi zingine zimepokelewa katika idara ya kongamano ambapo makala zilizofupishwa 179 zitachapishwa na makala kamili 15 zitawasilishwa katika kongamano hilo.
Amesema kati ya masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni mapinduzi ya Kiislamu, mwamko wa Kiislamu na utandawazi, serikali ya Imam Mahdi na Utandawazi, uhusiano wa kimataifa, sheria na utandawazi, utambulisho wa Kiislamu na utandawazi pamoja na changamoto na fursa zinazojitokeza.
Kongamano hilo litafanyika Februari 19 katika Ukumbi wa Shahid Mutahhari Chuo Kikuu cha Tarbiat Modaress.
954538