IQNA

Sheikh wa al Azhar aunga mkono kukatwa misaada ya Marekani kwa Misri

18:59 - February 18, 2012
Habari ID: 2276392
Sheikh wa al Azhar ameafiki suala la kukatwa misaada ya kifedha ya Marekani kwa Misri ikiwa ni ishara ya kupinga uingiliaji wa serikali ya Washington katika masuala ya ndani ya Misri.
Tovuti ya Almesryoon imemnukuu Sheikh Ahmad Tayyib akisema katika mazungumzo yake na Sheikh Muhammad Hassan ambaye ni miongoni mwa maulamaa wakubwa wa al Azhar akisema kuwa anaafikiana na pendekezo lake la kukatwa misaada ya kifedha ya Marekani kwa Misri.
Sheikh wa al Azha amesema hatua hiyo ni kielelezo cha jibu la taifa la Misri kwa njama zinazofanwa na Marekani kwa ajili ya kudumisha ushawishi wake nchini Misri baada ya mapinduzi ya wananchi.
Sheikh Ahmad Tayyib amewataka Wamisri wote wa ndani na nje ya nchi kuunga mkono pendekezo hilo.
Kwa upande wake Sheikh Muhammad Hassan amesema kuwa katika siku zijazo kutafanyika kikao cha kupasisha mipango ya kukatwa misaada ya Marekani kwa Misri. Kikao hicho kitahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Misri Kamal al Janzuri na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa nchi hiyo Fayza Abuol Naga. 955226


captcha