Benki hiyo ya Jaiz ilianza kazi jana mjini Abuja miezi 9 baada ya kupewa kibali cha kuendesha shughuli za kifedha kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Benki hiyo itafungua matawi katika miji mikubwa ya Nigeria ili kuwawezesha raia wa nchi hiyo kupata huduma za benki isiyokuwa ya riba.
Mkuu wa Benki Kuu ya Nigeria Lamido Sanusi Julai mwaka jana alitoa habari ya kuanzishwa Benki ya Kiislamu ya Jaiz nchini Nigeria lakini ufunguzi wa benki hiyo uliakhirishwa kutokana na upinzani wa baadhi ya makundi yasio ya Kiislamu.
Nigeria ambayo ni nguvu kubwa zaidi ya uchumi ya magharibi mwa Afrika, inataka kuwa kituo kikuu cha huduma za masuala ya kifedha-Kiislamu katika eneo hilo. 956030