IQNA

Kuwait yamfunga jela mwandishi aliyetusi Ushia

14:16 - February 20, 2012
Habari ID: 2277574
Mwandishi wa kisalafi wa Kuwait Muhammad al Malifi aliyemvunjia heshima Imam wa Zama Mahdi (as) amewekwa korokoroni.
Mahakama ya Kuwait jana Jumapili ilitangaza kuwa Muhammad al malifi amewekwa korokoroni kwa muda wa siku 21 kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi.
Mahakama ya Kuwait imetangaza kuwa Muhammad al Malifi anatuhumiwa kuvunjia heshima matukufu ya madhehebu ya Shia, kuvuruga umoja wa kitaifa na kueneza fitina za kimadhehebu.
Kikao cha kuchunguza mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya mtuhumiwa huyo kitafanyika leo na Muhammad al Malifi ataelezwa mashtaka yake katika kikao hicho.
Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Kuwait wamekuwa wakifanya maandamano katika siku kadhaa zilizopita wakionyesha upinzani wao dhidi ya mwenendo wa mtuhumiwa huyo na kutaka afikishwe mahakamani.
Vilevile Ayatullah Muhammad Baqir Muhri kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa Kuwait ametoa taarifa akimtaka Waziri wa Sheria wa nchi hiyo kumfungulia mashtaka Muahammad al Malifi na kusisitiza kuwa iwapo serikali haitachukua hatua za dharura Waislamu wataendeleza malalamiko na maandamao. 956732
captcha