Uchunguzi wa mwisho kuhusu ukarabati wa msikiti huo unafanywa na Halmashauri ya mji wa Madina na Kamati ya Ustawi ya mji huo mtukufu. Mradi huo umepasishwa na Wizara ya Wakfu ya Saudia.
Mpango huo unajumuisha kazi ya kuzidisha viwanja vya Msikiti wa Quba na maeneo ya kuegesha magari na kazi yote hiyo itagharimu riale milioni 100 za Saudi Arabia.
Jiwe la msingi la Msikiti wa Quba liliwekwa na Mtume Muhammad (saw) katika mwaka wa kwanza wa Hijria baada ya tu ya mtukufu huyo kuwasili mjini Madina akitokea Makka.
Msikiti huo umekarabatiwa mara kadhaa. Mara ya kwanza ilikuwa katika zama za utawala wa Othman bin Affan na mara ya mwisho ulikarabatiwa mwaka 1405 Hijria.957629