Kwa mujibu wa tovuti ya Bernama, maandamano hayo yaliyofanyika mara tu baada ya kusimamishwa swala ya Ijumaa yaliandaliwa na chama cha Kiislamu cha PAS.
Maelfu ya Wamalaysia walishiriki katika maandamano hayo ambapo walipiga nara za kulaani jeshi la Marekani na kutaka kitabu kitakatifu cha Qur'ani kiheshimiwe na kila mtu.
Sambamba na maandamano hayo, Waislamu wa Pakistan pia walifanya maandamano makubwa ya kulalamikia jambo hilo katika miji ya Lahore, Peshawar, Islamabad, Karachi na miji mingine muhimu ya nchi hiyo.
Siku ya Jumanne askari wa Marekani wanaohudumu katika kikosi cha NATO walichoma moto vitabu vingi wa Kiislamu kikiwemo kitabu kitakatifu cha Qur'ani, katika kambi yao ya kijeshi iliyoko huko Bagram, jambo ambalo limeamsha hasira kubwa ya watu wa Afghanistan na nchi nyingine za Kiislamu.
Kufuatia kuongezeka maandamano hayo ambayo yamepelekea Waafghanistan kadhaa kupoteza maisha yao, viongozi wa Marekani akiwemo John Allen, Kamanda wa NATO nchini Afghanistan, Leon Panetta, Waziri wa Ulinzi na Rais wa Barack Obama wa nchi hiyo wamewaomba radhi Waislamu kutokana na kitendo hicho cha kipumbavu cha askari wao huko Afghanistan. 959587