IQNA

14:51 - February 26, 2012
Habari ID: 2280767

Askari usalama wa Saudia wamkamata mkurugenzi wa tovuti ya Kishia

Askari usalama wa Saudia wamemtia nguvuni mkurugenzi wa tovuti ya Kishia inayojulikana kwa jina la Kanali ya Alfajiri ya Utamaduni kwa tuhuma za kujishughulisha na mambo yanayodhuru ufalme wa nchi hiyo.

Habib al-Maatiq ambaye ni mshairi na mpiga-picha mashuhuri wa Kishia wa Saudia ametiwa nguvuni kwa madai ya kuendesha na kusimamia tovuti ambayo eti inahatarisha maslahi ya utawala wa Saudia katika Mkoa wenye wakazi wengi wa Kishia wa Qatif.
Mara tu baada ya kutiwa nguvuni askari usalama wa nchi hiyo pia walifunga ofisi ya tovuti iliyotajwa. Wakati huohuo askari hao wamemtia nguvuni Husseini Malik as-Salaam, kijana mwingine wa Kishia ambaye ni mashuhuri kwa shughuli ya upigaji picha. Vyombo vya kuaminika vimetangaza kwamba as-Salaam alitoweka ghafla siku ya Jumatano iliyopita baada ya kukitembelea Chuo cha Ufundi cha mji wa al-Hubeil ambapo baadaye ilifahamika kuwa alikuwa ametiwa nguvuni na kufungwa jela na vyombo vya usalama vya Saudia.
Kijana mwingine wa Kishia kwa jina la Muhammad Salman al-Aqili alitiwa nguvuni na askari usalama wa Saudia Ijumaa iliyopita bila ya kutolewa sababu yoyote. 960043
captcha