IQNA

14:56 - March 11, 2012
Habari ID: 2289684

Utawala wa Saudia wawakandamiza Mashia ili kuwatisha Masuni

Gazeti moja la Marekani limeandika kwamba utawala wa Saudi Arabia unawakandamiza Mashia wa nchi hiyo kwa madhumuni ya kutia woga na kuwatisha Masuni ili nao wasije wakasimama dhidi ya utawala huo.

Likifafanua suala hilo, gazeti la Marekani la Foreign Policy limesisitiza kuwa siasa za utawala wa Saudia za kuwakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia ni sehemu muhimu ya sera za utawala huo. Limeandika kwamba katika miezi ya hivi karibuni utawala huo umeua kwa kuwapiga risasi vijana saba wa Kishia na kuwajeruhi wengine wengi mashariki mwa nchi hiyo, ambalo ni eneo lenye wakazi wengi wa Kishia.
Gazeti hilo la Marekani linasema kwamba licha ya kuwa maandamano kama yale yanayofanywa na Mashia wa Saudia yanaonekana katika nchi nyingine za Kiarabu na kuakisiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya habari vya nchi hizo na vya Kimataifa lakini vyombo hivyo hivyo vimepuuza na kufumbia macho maandamano ya Mashia wa Saudia na hivyo kuwaacha wakandamizwe kinyama na utawala wa nchi hiyo. Limeongeza kuwa utawala wa Riyadh unatumia madai yasiyo na msingi kwamba Mashia wa nchi hiyo wanatumiwa na Iran kutaka kudhibiti vyanzo vya mafuta vya nchi hiyo, ili kudumisha ukandamizaji wake dhidi ya wakazi hao wanaopigania haki zao za kimsingi na pia dhidi ya Masuni wa nchi hiyo.
Gazeti hilo la Marekani linasisitiza kwamba vyombo vya Kiarabu vimekuwa vikiituhumu Iran kuwa inaimarisha Ushia nchini Saudia, ili kwa njia hiyo kuwagonganisha wananchi wa nchi hiyo. Linasisitiza kwamba hizo ni siasa ambazo zimekuwa zikitekelezwa hivi karibuni pia na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.
Linamalizia kwa kuandika kuwa uingiliaji wa baraza hilo katika masuala ya ndani ya Bahrain umechochea sana tofauti za kimadhehebu katika Mashariki ya Kati. 969338
captcha