IQNA

Kituo cha Kiislamu Uingereza chalaani kushambuliwa msikiti Brussels

19:00 - March 17, 2012
Habari ID: 2293135
Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kimetoa taarifa kikilaani shambulizi lililofanywa dhidi ya Msikiti wa Imam Ridha (as) katika mji mkuu wa Ubelgiji huko Brussels na kumuua shahidi Imam wa msikiti huo.
Taarifa ya kituo hicho imelaani kitendo hicho cha kinyama kilichofanywa ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu na mtu mwenye misimamo mikali na asiyejua dini na kumuuwa Hujjatul Islam Walmuslimin Sheikh Abdullah Dahduh na imeitaka serikali ya Ubelgiji kutoa adhabu kali kwa watu waliohusika na jinai hiyo. Vilevile imetoa wito wa kushughulikiwa wale waliounga mkono na kupigia debe kitendo hicho cha kidhalimu.
Taarifa ya Kituo cha Kiislamu cha Uingereza pia imewataka maulama wa Kiislamu walaani jinai hiyo ya kinyama ambayo haioani na sheria zote za Mwenyezi Mungu.
Imesisitiza kuwa Uislamu umetuhimiza kustahamiliana na kuheshimu itikadi za watu wengine na kwa msingi huo tunalazimika kueneza utamaduni huo.
Wakati huo huo polisi ya Ubelgiji imetangaza kuwa imemtia nguvuni mtu mmoja mwenye umri wa miaka 47 kwa kuhusika na tukio la kuchomwa moto Msikiti wa Imam Ridha (as) na kwamba mtu huyo amekiri kutenda jinai hiyo. 973220
captcha