Washiriki katika kikao cha viongozi wa kidini nchini Ufaransa wametoa taarifa wakilaani vitendo vya baadhi ya wagombea urais wa nchi hiyo vya kutumia vibaya masuala ya kidini katika kampenzi zao.
taarifa hiyo imetiwa saini na viongozi wa dini za Kikristo, Uislamu, Uyahudi na Budha.
Imesema kuwa viongozi wa dini mbalimbali nchini Ufaransa hawana nia ya kuzungumzia mjadala wa nyama halali au iliyochinjwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na Kiyahudi unaotawala sasa katika vyombo vya habari lakini wanaamini kuwa umewadia wakati wa kutiliwa maanani nafasi ya masuala ya kidini katika jamii.
Taarifa hiyo imesena viongozi wa kidini wa Ufaransa wanawataka wagombea kiti cha rais kukomesha mjadala juu ya dini na kushughulikia matatizo halisi ya jamii. 973786