IQNA

Wakristo wa New York waandamana kupinga wapagani

12:13 - March 25, 2012
Habari ID: 2294534
Wakristo wa mji wa New York nchini Marekani walifanya maandamano jana wakipinga kitendo cha watu wasiomwamini Mungu cha kukana kuwepo Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Tovuti ya Mooslym.com imeripoti kuwa, kundi la watu wasioamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu limeweka bango lenye maandishi yanayovunjia heshima itikadi za dini zinazomwamimi Mwenyezi Mungu Muumba juu ya dula la kuuza pombe na vileo na kukana kuwepo kwake, jambo ambalo limewakasirisha mno Waislamu na Wakristo wa mji wa New York.
Arther Thomas, Mkristo wenye umri wa miaka 60 wa New York, amesema kuwa hatua hiyo ni ya kijinga na kukana kuwepo Mwenyezi Mungu kupitia njia ya kuvunjia heshima itikadi za dini ya Kiislamu ni kuwavunjia heshima pia watu wote wanaomwamini Mungu Mmoja wakiwemo Wakristo.
Mshiriki mwingine katika maandamano hayo amesema kundi hilo la wapagani linakana kuwepo kwa Mwenyezi Mungu lakini linasahau kuwa kumkana Mungu kunapalilia njia ya shetani katika nyoyo zao.
Wakristo wa mji huo pia wamelitaka jeshi la polisi kutoa amri ya kuondolewa bango hilo linalovunjia heshima matukufu ya kidini lililotundikwa na wapinzani wa dini katika moja ya mitaa ya mji huo. 973933

captcha