IQNA

Watunisia walaani kuchanwa Qur'ani

12:43 - March 26, 2012
Habari ID: 2294810
Maelfu ya wananchi wa Tunisia wameandamana wakitaka kuundwa serikali ya Kiislamu nchini mwao.
Wananchi hao waliandamana jana katika mji mkuu Tunis wakitaka Sheria za Kiislamu zitawale nchini humo na vilevile wamelaani kuvunjiwa heshima matukufu ya Waislamu.
Kaulimbiu za wanaandamanaji hao wa Tunisia zilikuwa ni "Wananchi wanataka serikali ya Kiislamu" na "Wananchi wanataka Sheria za Kiislamu."
Waandamanaji hao pia wamelaani vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na maeneo matakatifu ya Waislamu wakisisitiza kuwa hizo ni jinai zisizosameheka.
Itakumbukwa kuwa, watu wenye chuki na Uislamu tarehe 15 mwezi huu wa Machi walivamia misikiti kadhaa huko Ben Gardan, kusini mwa Tunisia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Libya na kuchana nakala kadhaa za Qur'ani Tukufu.
974732


captcha