IQNA

Pendekezo la kuongezwa neno la "Laa Ilaha Illallah" katika bendera ya Tunisia

12:29 - April 02, 2012
Habari ID: 2296430
Chama cha Kitaifa cha Tunisia kimetoa pendekezo la kuongezwa neno la Laa Ilaha Illallah katika bendera ya nchi hiyo.
Mwakilishi wa chama hicho Ibrahim Hamdi amewataka mawaziri wa serikali ya nchi hiyo wachunguze pendekezo la kuongezwa neno la Laa Ilaha Illallah katika bendera ya Tunisia. Amesema katika kikao hicho kilichohudhuriwa na mawaziri kadhaa wa serikali ya Tunis kwamba Tunisia ni nchi ya Kiislamu na kwa kutulia maanani utambulisho wa kitaifa na kidini wa raia wake na ili kuonyesha uungaji mkono wetu kwa Uislamu na Waislamu tunapaswa kuweka neno la Laa Ilaha Illallah katika bendera ya faifa.
Mwakilishi huyo wa Bunge la Tunisia amelitaka Bunge la Waasisi kuchunguza pendekezo hilo kwa undani na kuongeza neno hilo juu ya hilali iliyoko kwenye bendera ya nchi hiyo ili kuunga mkono mapinduzi ya wananchi. 976928

captcha