Nuruddin al Khadimi amesema kuwa si sahihi misikiti hiyo kutumiwa kama majukwaa ya kisiasa na kwamba maeneo hayo ya ibada yanapaswa kutumiwa kwa ajili ya kueneza uvumilivu na hali ya kuheshimiana katika jamii.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Tunisia amesema kuwa karibu misikiti 400 kati ya elfu 5 ya nchi hiyo inadhibitiwa na wafuasi wa kindi la Mawahabi na kuna matatizo mengi katika misikiti 50.
Al Khadimi amesema kuwa mwaka jana Mawahabi walidhibiti moja ya misikiti mikuu ya mji wa Sidi Bouzid ambako ndiko yalikoanzia mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo na kuupachika jina la "Qandahar", ngome kuu ya wapiganaji wa Taliban huko Afghanistan.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Tunisia amesisitiza kuwa miezi kadhaa ilioyopita Mawahabi walimfukuza Imam wa Msikiti wa Bilal katika eneo la Aryana nchini Tunisia na kulifanya eneo hilo la ibada kuwa kituo cha kueneza fikra za Kiwahabi. 977016