IQNA

Mgombea Urais wa Ikhwani aahidi kutekeleza sheria za Kiislamu Misri

16:57 - April 07, 2012
Habari ID: 2299461
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Ikhwanul Muslimin nchini Misri amesema lengo lake kuu ni kutekeleza sheria za Kiislamu nchini humo iwapo atashinda uchaguzi ujao.
Khairat al-Shater ameahidi pia kuifanyia marekebisho makubwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ambayo ilikuwa na nafasi kubwa katika kukandamiza wapinzani wakati wa utawala uliong'olewa madarakani. Amesema ataunda tume maalumu itakayosaidia Bunge kuhakikisha kwamba sheria za Kiislamu zinatekelezwa nchini Misri.
Al Shater ambaye ni mfanyabiashara milionea anatazamiwa kukabidhi nyaraka zake za kujiandikisha kwa ajili ya kugombea urais hii leo Alkhamisi.
Uamuzi wa mwanasiasa huyo ambaye alitiwa jela mara nyingi wakati wa utawala wa dikteta wa zamani wa Misri Hosni Mubarak, wa kugombea kiti cha Rais nchini Misri umezitia wasiwasi mkubwa nchi za Magharibi ambazo zina hofu kutokana na kupanda nyota ya harakati za Kiislamu nchini Misri.
979639

captcha