Tovuti ya "islamicstudies.harvard" imeripoti kuwa kongamano hilo linasimamiwa na Chuo Kikuu cha Harvard kwa shabaha ya kuchunguza hali na uzoefu wa Waislamu wenye asili ya Afrika wa Marekani nchini humo.
Masuala mengine yanayochunguzwa ni pamoja na matatizo ya Waislamu hao, hali ya wanawake Waislamu wenye asili ya Afrika raia wa Marekani, jamii za Kiafrika- Kimarekani zinazofuata madhehebu ya Shia, utamaduni wa Kiafrika na Kimarekani katika mtazamo wa Uislamu, kigezo kipya cha uongozi wa jamii za Kiislamu na uongozi wa Kiislamu katika jamii za Kiafrika-Kimarekani.
Kongamano hilo litakamilisha kazi zake kesho. 980149