Tovuti ya Daily Targum imeripoti kuwa wiki ya Ujue Uislamu inasimamiwa na Jumuiya ya Wanachuo Waislamu wa Chuo Kikuu cha Rutgers kwa shabaha ya kuarifisha utamaduni wa Kiislamu na kupanua mazungumzo ya kidini na kijamii kati ya wanachuo Waislamu na wasio Waislamu.
Programu hiyo itaendelea kutekelezwa hadi tarehe 13 Aprili na katika kipindi hicho chote wanafunzi wa chuo hicho wanaweza kuwasilisha maswali yao kuhusu Uislamu na Waislamu.
Ajenda nyingine ya mpango huo ni hotuba mbalimbali zinazohusiana na uadilifu wa kijamii wa Waislamu, ubaguzi wa kimbari, umaskini, matatizo ya kiuchumi, mapinduzi yaliyotokea katika nchi za Mashariki ya Kati na uhuru na sheria katika Uislamu. 981811