Ofisi ya IQNA tawi la Afrika imeripoti kuwa masomo hayo yamehudhuriwa na mashekhe Qasim Abdulsalam, Abdul Muttalib, Sulaiman Issa, Yusuf Munir na Muhammad Mukasa ambao ni wahitimu wa Chuo Kikuu cha al Mustafa katika mji mtakatifu wa Qum.
Katika masomo hayo kulichunguzwa na kutolewa mafunzo juu ya mbinu za uendeshaji sahihi wa misikiti na shule za kidini.
Mwishoni mwa masomo hayo washiriki watatembelea Kituo cha Kiislamu na Shule ya Mayatima ya Imam Ridha (as) na Madrasa ya Imam Sadiq (as) katika viunga vya jiji la Kampala.
Mafunzo hayo yalianza Alkhamisi iliyopita na yatakamilika kesho kwa sherehe rasmi na kutolewa zawadi kwa washiriki. 982581