IQNA

Semina ya "Wajibu wa Mwanamke Muislamu katika Kuanzisha Jamii ya Kiqur'ani" kufanyika India

18:27 - April 14, 2012
Habari ID: 2304546
Semina itakayochunguza wajibu na nafasi ya wanawake Waislamu katika kuanzisha jamii ya Kiqur'ani itafanyika kesho katika mi wa Lucknow katika jimbo la Utta Pradesh nchini India. Semina hiyo inasimamiwa na Taasisi ya Qur'ani ya mji wa Lucknow.
Ripota wa IQNA huko kusini magharibi mwa Asia Qamar Alim amesema kuwa Taasisi ya Qur'ani ya Lucknow imetangaza kuwa semina hiyo itachunguza wajibu wa wanawake Waislamu katika kuanzisha jamii ya Kiqur'ani na kutoa malezi sahihi kwa mujibu wa mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu na Suna za Mtume Muhammad (saw).
Semina hiyo itahutubiwa na Safia Nasim ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Waislamu wa Lucknow, Bi Ghazala Afzur kutoka mji wa Gonda na Bi Rabia ambaye ni miongoni mwa wasimamizi wa semina hiyo.
Wanawake wote wa mji wa Lucknow wamealikwa kushiriki katika semina hiyo kwa shabaha ya kujifunza utamaduni na maarifa ya Qur'ani Tukufu juu ya jinsi ya kulea kizazi bora. 984812

captcha