IQNA

Miujiza ya kisayansi ya Qur'ani ni ithbati kuwa Uislamu ndio njia sahihi

22:42 - April 15, 2012
Habari ID: 2304945
Moja ya njia za kumkomboa mwanadamu wa dunia ya leo kutoka kwenye migogoro inayomkabili ni kumuongoza kuelekea katika miujiza ya Qur'ani Tukufu ili aweze kupata muongozo wa kweli ambao ni Uislamu, amesema mwanazuoni wa Misri.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Zaqul Raqeb Najjar ameyasema hayo katika makala yenye anwani ya 'Ishara ya Kiontolojia katika Qur'ani na Umuhimu wa Kisayansi wa Ishara Hizo'.
Katika makala yake, Najjar amesisitiza kuwa miujiza ya kisayansi ya Qur'ani ni ushahidi tosha kuhusu ukweli wa Uislamu.
Ameandika kuwa: 'Katika dunia ya leo, vyombo vingi vya habari vinaendeshwa na makundi ya lobi ya Wazayuni ambao wanatumia vyombo hivyo vya habari kupotosha imani, maadili bora na mila za jamii ya mwanadamu. Kwa hivyo kuna haja kubwa kwa Waislamu kuarifisha Uislamu halisi duniani na kukabiliana na njama za kuharibu sura ya Uislamu.'
Kwa mujibu wa Sheikh Najja, ustawi wa sayansi umeweza kubainisha wazi baadhi ya miujiza ya Qur'ani Tukufu na jambo hilo linaweza kutumika katika kuwajulisha walimwengu nuru ya Qur'ani.
Ametaja aya za Qur'ani kuhusu masuala ya kimaumbile kama vile kuumbwa bingu, maji, chimbuko la dunia, kiinitete cha mwanaadamu n.k na kusema wale waliofanya utafiti kuhusu miujiza ya Qur'ani wanasema kitabu hicho kitakatifu kimeashiria masuala kama hayo mara 1000 katika zaidi ya sura 40.
Sheikh Zaqul Raqeb Najjar alizaliwa mwaka 1933 na ni mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu ambaye amefanya juhudi tele za kuarifisha utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu duniani.
Hivi sasa yeye ni mkuu wa Kamati ya Muujiza wa Qur'ani na Sunah katika Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Misri.
982849
captcha