IQNA

Masomo ya Uislamu na Ufanisi wa Mwanadamu yamalizika Madagascar

23:58 - April 16, 2012
Habari ID: 2306314
Masomo ya Uislamu na Ufanisi wa Mwanadamu kwa ajili ya watu walioingia katika dini tukufu ya Kiislamu yamemalizika katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
Masomo hayo yamesimamiwa na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa al Mustafa cha Qum nchini Iran kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Masomo hayo yametolewa na Salim Ali Yusuf na Hurr Hussein, walimu wa teolojia ya Kiislamu ambao walijibu maswali ya washiriki katika nyanja mbalimbali za kidini.
Lengo la kutolewa masomo hayo ni kuimarisha misingi ya itikadi za Kiislamu kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliosilimu na kukubalidi dini ya Kiislamu hivi karibuni. 987001
captcha