IQNA

Mgombea aliyekataliwa wa Ikhwani awasilisha malalamiko

23:58 - April 16, 2012
Habari ID: 2306318
Mgombea wa kiti cha rais aliyekataliwa na Kamisheni Kuu ya Uchaguzi ya Misri kheirat al Shater amewasilisha malalamiko yake kwa kamisheni hiyo.
Al Shatir amewasilisha malalamiko hayo baada ya kuondolewa katika orodha ya wagombea wa uchaguzi ujao wa rais wa Misri.
Awali Kamisheni Kuu ya Uchaguzi ya Misri ilikuwa imewaondoa wagombea wengine katika orodha hiyo akiwemo kiongozi wa chama cha al Ghad Aiman Nour na Umar Suleiman aliyekuwa mkuu wa vyombo vya ujasusi katika utawala uliong’olewa madarakani wa Hosni Mubarak kwa sababu za kutotimiza masharti ya kugombea.
Hadi sasa katibu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Amru Mussa, Abdul Minim Abul Futouh aliyewahi kuwa miongoni mwa viongozi wa Ikhwanul Muslimin na Ahmad Shafiq, waziri mkuu wa zamani wa Misri wamepasishwa kwa ajili ya kugombea kiti cha rais wa Misri.
Uchaguzi wa rais wa Misri umepangwa kufanyika tarehe 23 na 24 Mei. 987182

captcha