IQNA

Ban Ki-moon aitaka Bahrain kuheshimu haki za raia

21:21 - April 17, 2012
Habari ID: 2307103
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa serikali ya Bahrain kuheshimu haki za wananchi wa nchi hiyo na kuwaruhusu kuandamana kwa amani.
Ban Ki-moon amesema kuwa taifa la Bahrain lina haki ya kufanya maandamano kwa uhuru na kwamba viongozi wa utawala wa Aal Khalifa wanapaswa kuheshimu haki za wananchi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka pia viongozi wa Bahrain kuruhusu mwanahakati wa kutetea haki za binadamu Abdulhadi al Khawaja anayeshikiliwa katika jela za utawala wa nchi hiyo ahamishiwe nchini Denmark. Khawaja anafanya mgomo wa kula kwa kipindi cha miezi miwili sasa akipinga ukatili unaoendelea kufanywa na utawala wa Bahrain dhidi ya raia wanaopinga serikali ya kifalme ya nchi hiyo.
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeilaumu vikali serikali ya Bahrain kwa kuwakandamiza kinyama raia wanaoandamana kwa amani. Shirika hilo limetoa ripoti mpya mjini London likisisitiza kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Bahrain ungali unaendelea. 987832

captcha