Katibu Mkuu wa Jumuiya ya al Wifaq Sheikh Ali Salman amesema kuwa Marekani imekuwa na msimamo dhaifu kuhusu masuala ya Bahrain na imepuuza ukweli wa mambo kuhusu haki za wananchi na uhakika kuhusu mambo mbalimbali ya nchi hiyo.
Sheikh Ali Salman ameitaka jamii ya kimataifa kuwa pamoja na mataifa na kujiweka mbali na madikteta na kusisitiza kuwa jumuiya hiyo itaendeleza uhusiano wake na nchi za Kiarabu na katika uga wa kimataifa kwa ajili ya kutangaza mitazamo ya wapinzani wa Bahrain.
Amesema kuwa jumuiya hiyo itaendelea kuunga mkono maandamano ya amani wa wananchi kwani utawala wa kifalme wa Aal Khalifa unataka kuziba midomo ya wananchi. Amesisitiza kuwa utawala wa Aal Khalifa unapinga marekebisho na hauko tayari kwa ajili ya mazungumzo ya kweli na kambi ya upinzani. 988483