Husseiniya ya Kwanza ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Misri imefunguliwa mjini Cairo kwa kuhudhuriwa na Sheikh Ali Kurani, mwanazuoni mashuhuri wa Lebanon, ambaye amekuwa akiishi kwa miaka mingi katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
Kwa mujibu wa tovuti ya shabab.ahram, semina ya kidini na kiutamaduni pia imefanyika pambizoni mwa sherehe za ufufunguzi wa Husseiniya hiyo.
Baada ya kulakiwa na umati mkubwa wa Waislamu katika uwanja wa ndege wa mjini Cairo, Sheikh Kurani katika safari yake ya siku kadhaa mjini humo amekutana na kuzungumza na idadi kubwa ya Mashia wa Misri wakiwemo shakhsia wa masuala ya kidini na kiutamaduni na vilevile wanazuoni mashuhuri wa nchi hiyo.
Katika upande wa pili baadhi ya makundi yaliyo na chuki dhidi ya Ushia ya Misri yamekosoa vikali safari ya mwanazuoni huyo nchini humo na kudai kwamba Mashia wanataka kutumia vibaya hali ya kisiasa ya nchi hiyo kwa maslahi yao binafsi. 1002292