Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kwamba nchi za Magharibi zinafanya njama za kuipindua serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria kwa kuwa nchi hiyo inaunga mkono makundi ya muqawama.
Sayyid Hassan Nasrullah aidha amesema, Marekani, nchi za Magharibi, Israel pamoja na baadhi ya pande za eneo zinataka kuipindua serikali ya Syria kwa sababu tu zinataka kusiweko na serikali ambayo ni muunga mkono mkubwa wa mapambano ya Lebanon na Palestina dhidi ya Israel na ubeberu.
Aidha Nasrullah amesema, watu wanaofanya mashambulizi ya kigaidi na kuleta machafuko nchini Iraq, ndio hao hao wanaotaka kuharibu hali ya mambo ya Syria.
Vilevile Katibu Mkuu wa Chama cha Hizbullah cha Lebanon amezikosoa baadhi ya nchi za Kiarabu kwa kutuma magaidi nchini Syria ili wakaripue mabomu na kuua watu wasio na hatia nchini humo.
1005410