IQNA

12:13 - May 12, 2012
Habari ID: 2323692

Mwakilishi wa OIC aelekea Thailand kutatua matatizo ya Waislamu

Sayyid Qassim al-Masri, mshauri wa Ikmal Deen Ihsanoughlu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC kesho Jumapili ataelekea nchini Thailand kwa lengo la kutatua baadhi ya matatizo yanayowakabiliwa Waislamu wa nchi hiyo.

Matatizo na mvutano mkubwa umezuka baina ya serikali na Waislamu wa nchi hiyo wanaohisi kuwa serikali inawakandamiza na kuwabagua kuhusiana na masuala mengi. Waislamu wengi wa Thailand wanaishi kusini mwa nchi hiyo. Hiyo itakuwa ni safari ya tatu kufanywa na ujumbe wa ngazi za juu wa OIC nchini Thailand tokea mwaka 2005 kwa ajili ya kushughuliki amasuala ya Waislamu. 1004101
captcha