IQNA

Sherehe za kuadhimisha uzawa wa Imam Ali (as) kufanyika Uingereza

18:27 - May 15, 2012
Habari ID: 2326727
Sherehe za kuadhimisha uzawa wa Imam Ali (as) zimepangwa kufanyika Juni Nne inayosadifiana na tarehe 13 Rajab katika Kituo cha Kiislamu huko London nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa tovuti ya ic-el sherehe hizo zitakazoanza saa moja jioni kwa wakati wa Uingereza zitajumuisha ratiba mbalimbali ambazo zimeandaliwa na Kituo cha Kiislamu kwa ajili ya kuwatumbuiza Mashia na wapenzi wa Imam huyo mtukufu. Kituo hichohicho cha Kiislamu kimeratibu sherehe nyingine kama hizo ambazo zitafanyika tarehe 18 Juni sawa na tarehe 27 Rajab kwa shabaha ya kuadhimisha siku ya kubaathiwa Bwana Mtume (saw). Siku ya kuzaliwa Imam Hussein (as) pia imepangwa kusherehekewa katika kituo hicho tarehe 23 Juni sawa na tarehe 3 Shaban. Tunaashria hapa kwamba kituo hicho pia kimepanga kuandaa mkutano wa kimataifa wa kila mwaka ambao hufanyika kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Khomeini (MA) hapo tarehe 3 Juni. Kikao hicho kitajadili fikra za Imam Khomeini kuhusiana na masuala tofauti. 1008422
captcha