IQNA

Kibali cha kujengwa shule ya Kiislamu mjini Brussels chatolewa

18:27 - May 15, 2012
Habari ID: 2326728
Kibali cha kujengwa shule ya Kiislamu itakayotoa mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya msingi huko Brussels mji mkuu wa Ubelgiji kimetolewa na wakuu wa nchi hiyo.
Vibali kama hivyo vimetolewa kwa ajili ya kujengwa shule kama hizo katika miji mingine ya nchi hiyo lakini hii ni mara ya kwanza kwa kibali cha kujengwa shule ya aina hiyo ya Kiislamu katika mji mkuu kutolewa. Mpango wa kujengwa shule hiyo uliwasilishwa kwa viongozi wa serikali na taasisi ya Kiislamu ya Ubelgiji ya al-Amal kutokana na watoto wa Kiislamu wa mji huo kuzuiwa kushiriki masomo katika shule nyingine za kawaida za mji huo wakiwa wamevalia hijabu. Kuthibiti jambo hilo kutawahakikishia wazazi wa Kiislamu kuwa watoto wao watapata masomo yanayofaa wakiwa katika mazingira ya Kiislamu yanayoambatana na sheria za Kiislamu. Taasisi ya al-Amal ilianzishwa na wahajiri wa Kiislamu kutoka Morocco na kuna msikiti unaoitwa kwa jina hilohilo pembeni ya taasisi hiyo. 1008418
captcha