Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA jarida hilo ambalo limetayarisha na Taaisi ya Ustawi wa Utafiti wa Kisayansi katika ISESCO linajumuisha makala 11 za kisayansi ambazo zimeandikwa na wasomo kutoka Mali, Sudan, Malaysia, Iran, Tunisia, Algeria, India na Bangladesh.
Makala hizo zinahusu masuala kama vile utumizi bora wa nishati katika sekta ya kilimo, uboreshaji ardhi za kilimo, viwango bora katika uzalishaji madawa n.k.
Jarida hilo huchapishwa kila mwaka mara mbili kwa lugha ya Kiingereza ambapo wanasayanis kutoka nchi wanachama hupewa fursa ya kuwasilisha makala kuhusua masuala mbali mbali ya kisayansi. Jarida hilo pia linapatikana kwa njia ya kieletroniki kupitia anuania ifuatayo: www.icpsr.org.ma
1009664