Akizungumzia suala hilo, Hujjatul Islam wal Muslimin Ismail Pirnia, mwakilishi wa Jamiatul Mustafa al-Aalamiya nchini Madagascar amesema kwamba sherehe hizo zilihudhuriwa na shakhisa mbalimbali wa kidini na masuala ya kiutamaduni akiwemo Ayatullah Husseini Qazwini, Mkuu wa Televisheni ya Kimataifa ya Wilayat ambaye pia ni mhadhiri mashuhuri wa masuala ya kidini nchini Iran. wanafunzi waliovishwa vilemba katika sherehe hizo walihitimu masomo yao katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wengine katika Madrasa ya Imam Swadiq nchini Madagascar. Wanafunzi hao watatumwa katika pembe mbalimbali za Madagascar kwa ajili ya kuendesha tablighi na masomo ya kidini katika sehemu hizo. Shakhsia mbalimbali wa Madagascar pia walihudhuria shehere hizo. 1012452