Shakhsia mbalimbali wa kidini na kiutamaduni wakiwemo Ayatullah Husseini Qazwini, Mkurugenzi wa Televisheni ya Kimataifa ya Wilayat ambaye pia ni mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Waliasr (af), Hujjatul Islam wal Muslimin Ismail Pirnia, mwakilishi wa Jamiatul Mustafa al-Alamiya nchini Madagascar, Sheikh Adam, Mkuu wa Taasisi ya Answar Ahlul Beit (as), Sheikh Abdu Rahman, Mkurugenzi wa Redio Majunga, Sheikh Jaafar, Mkurugenzi wa Redio Tuliar pamoja na wanafunzi na mashekhe wengine 60 mashuhuri wa nchi hiyo. Katika sheherhe hizo, Ayatullah Hussein Qazwini alibainisha nafasi ya mwanamke katika Uislamu, taathira yake ya moja kwa moja kwa malezi ya watoto, fadhila zake za kimaadili pamoja na shakhsia na maisha ya Bibi Fatma Zahra (as) binti mtukufu wa Mtume (saw) katika Uislamu. Katika sherehe hizo, Swabahi Garaghani, mkuu wa Madrasa ya Tahura alibainisha mbinu zilizotumiwa na Bibi Zahra Mardhiya (as) katika kuwalea wanawe na kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wake kuhusiana na suala hilo. Mwishoni mwa sherehe hizo, Ayatullah Qazwini aliwapa zawadi wanawake wa walimu na wanafunzi wa kike wa Madrasa ya Tahura pamoja na wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule hiyo. 1012560