IQNA

Kuteuliwa Karbala kuwa mji mkuu wa utalii wa Kiislamu mwaka 2015

18:00 - May 21, 2012
Habari ID: 2330991
Mkuu wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mahoteli na Mikahawa ya Kitalii mjini Karbala ametaka kuchaguliwa mji huo mtakatifu kuwa mji mkuu wa utalii wa Kiislamu mwaka 2015.
Huku akiashiria maendeleo makubwa yaliyopatika katika mji huo katika sekta ya utalii na pia kuhusu miradi ya ujenzi wa miundombinu katika miaka ya hivi karibuni, Muhammd Swadiq al-Hur amewataka viongozi husika katika Wizara ya Utalii ya Iraq kuuchagua mji huo kuwa mji mkuu wa utalii wa kidini na Kiislamu katika mwaka 2015. Amesema tayari wakuu wa Karbala wametiliana saini na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kuongeza idadi ya wafanyaziara wa Iran wanaoutembelea mji huo mtakatifu. Amesema mji huo ndio ulio na hoteli nyingi zaidi za kuwapokea wageni wanaozuru Iraq na kwamba katika hali ya hivi sasa kuna hoteli zipatazo 400 ambapo 300 kati ya hizo zina vibali rasmi vya kujihusisha na masuala ya kutoa huduma kwa wageni wanaozuru mji huo. Amesema hoteli 100 zinafanya shughuli hiyo bila kuwa na vibali rasmi na kwamba nyingine nyingi zinaendelea kujengwa. Amesema hoteli nyingi za mji huo zina nafasi kubwa ya kuegezea magari kiasi kwamba kila hoteli ina nafasi inayowezesha mabasi 15 kuegezwa humo. 1012074
captcha