Ayatullah Ahmad Khatami, khatibu wa muda wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema hayo katika khutba za sala ya Ijumaa ya leo na kuongeza kuwa, taifa la Iran linatambua kuwa teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani ni haki ya kila mtu, na kwa ajili hiyo Iran haitotetereka hata kidogo katika misimamo yake.
Akiashiria kauli ya uongo ya Wamagharibi katika ahadi waliyoitoa miaka mitatu iliyopita kuwa wangedhaminia Iran fueli nyuklia amesema, tangu wakati huo hadi hivi sasa vijana wa Kiirani wameliwezesha taifa hili kujizalishia lenyewe kiwango cha urani kilichokuwa kimeahidiwa na Wamagharibi hao baada ya Wamagharibi kuvunja ahadi zao kwa Iran.
Aidha amezungumzia fatwa ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya kuharamisha matumizi ya silaha za atomiki na kuongeza kuwa, ili kuuhakikishia ulimwengu kuwa Iran haina nia ya kuunda silaha hizo, Tehran imekuwa ikiwaalika mara kwa mara wakaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kukagua vinu vyake vya nishati ya nyuklia na kwamba, hata wakaguzi hao nao wameshindwa kupata jambo lolote linaloweza kuthibitisha kuwa Iran imekwenda kinyume na miradi ya amani ya nyuklia.
1016158