IQNA

12:11 - May 28, 2012
Habari ID: 2335940

Qatar, mwenyeji wa kikao cha tisa cha Ulimwengu wa Kiislamu na Marekani

Kikao cha tisa cha Ulimwengu wa Kiislamu na Marekani kimepangwa kufanyika tarehe tarehe 29 hadi 31 Mei huko Doha mji mkuu wa Qatar.

Kwa mujibu wa tovuti ya OIC kikao hicho ambacho kinadhaminiwa na serikali ya Doha kitafanyika chini ya kauli mbiu ya ' Sauti Mpya, Peo Mpya.' Msemaji wa Ikmal Deen Ihsanoghlu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC anatazamiwa kufungua kikao hicho hapo kesho Jumanne. Viongozi na wawakilishi wa nchi tofauti za Kiislamu wanatazamiwa kushiriki kwenye kikao hicho ambacho kitajadili hali mpya ya kisiasa katika nchi za Kiarabu, mambo yanayotoa msukumo wa maendeleo na mabadiliko ya kiutamaduni ulimwenguni pamoja na masuala mengine muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu. 1018353
captcha