Amnesty imetoa wito huo katika ripoti yake yenye anuani ya: 'Sauti za Wapinzani Zabanwa Mkoa wa Mashariki'.
Ripoti hiyo imeutaka ufalme wa kiimla Saudia uwaachilie wafungwa hao wanaoshikiliwa bila kufunguliwa mashtaka na ambao aghalabu ni wa madhehebu ya Shia.
Amnesty imesema mamia ya watu wakiwemo watoto wametiwa nguvuni Saudi Arabia tokea Machi 2011.
Eneo la Mashariki mwa Saudi Arabia limekuwa medani ya maandamano dhidi ya ufalme tokea Februari mwaka 2011 ambapo waandamanaji wanataka haki za binaadamu ziheshimiwe. Aidha Wasaudi wanataka marekebisho ya kisiasa, uhuru wa manoni na kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa. Harakati za wananchi katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Mashariki mwa Saudia ni katika fremu ya mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa kote Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
1018476