Kongamano hilo linafanyika kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 23 tokea aage dunia Imam Khomeini (MA), mwanzilishi wa mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kikao hicho kitahudhuriwa na shakhsia muhimu wa kisiasa, kiutamduni, kielimu na kijamii wa Pakistan akiwemo spika wa bunge la Punjab, mkuu wa Harakati ya Minhaj al-Qur'ani, mkuu wa Chuo cha Kidini cha Jamiatul Muntadhar, mkuu wa Chuo cha Kidini cha Urwatul Wuth'qa, Mkuu wa Chuo cha Ridhawiya, Chuo cha Minhajul Hussein na shakhsia wengine wengi wanaompenda Imam Khomeini (as). Tunaashiria hapa kwamba maonyesho ya picha zinazohusiana na vipindi tofauti vya maisha ya Imam Khomeini yatafanyika pambizoni mwa kongamano hilo.1020352