Hizbullah imesema kuna dalili na ishara za kutosha zinazothibitisha kwamba magaidi wasio na huruma na watenda jinai ndio waliohusika nao. Imesema magaidi hao ni walewale vibaraka wanaoshirikiana na majasusi wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi kwa ajili ya kutenda jinai dhidi ya watu wasio na hatia wa Iraq. Taarifa ya Hizbullah imeendelea kusema kuwa magaidi hao wanajishughulisha na jinai mchana na usiku kwa lengo la kupanda mbegu ya fitina katika jamii ya Iraq na kujaribu kuwasha moto wa kimadhehebu na kidini utakaoteketeza eneo zima la Mashariki ya Kati. Huku ikilaani vikali shambulio hilo la kigaidi, Hizbullah imewataka watu wote wa Iraq kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ili kuwapokonya magaidi hao na viongozi wao fursa ya kutaka kuvuruga zaidi hali ya mambo nchini humo. Hizbullah imewataka Wairaqi wote kuzingatia umoja na mfungamano wao wa kitaifa ili kuwapokonya Wamagharibi fursa ya kutaka kuifanya nchi hiyo kuwa uwanja wa kutekelezea njama zao hatari dhidi ya Waislamu. Hizbullah mwishoni mwa taarifa hiyo imetoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa mlipuko huo wa kigaidi na kumwomba Mwenyezi Mungu azipe subira pamoja na kuwatakia nafuu na kupona haraka wale wote waliojeruhiwa katika mkasa huo. 1023049