Wasomi na wanafikra mashuhuri wa Pakistan walishiriki kwenye kongamano hilo lilioanza saa nne mchana kwa wakati wa nchi hiyo. Baadhi ya shakhsia waliozungumza katika kongamano hilo walisisitiza juu ya udharura wa kuzingatiwa mafundisho na tahamani za Kiislamu katika jamii hasa katika kipindi hiki ambacho maadui wa Uislamu wamekuwa wakitekeleza njama hatari kwa ajili ya kuudhoofisha Uislamu. Wamesema nchi za Kiislamu kama vile Pakistan ambazo zinajivunia Uislamu wao zimekuwa zikishambuliwa na kujuhumiwa kwa propaganda za maadui wa Uislamu ili kuzifanya zilegeze misimamo yao na kusalimu amri mbele ya utamaduni wa Magharibi.1023002