IQNA

18:04 - June 09, 2012
Habari ID: 2342927

Sehemu ya swala ya Waislamu nchini Ufaransa kubadilishwa kuwa kituo cha polisi

Meya wa mji wa Nice nchini Ufaransa amesema kuwa nyumba unayotumiwa na Waislamu kusimamisha swala za jamaa katika mji huo itabadilishwa kuwa kituo cha polisi.

Akijaribu kuhalalisha hatua hiyo meya huyo amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuwa nyumba hiyo inatumiwa kama sehemu ya kusimamishia swala bila kuwa ni kibali rasmi na kwamba imejengwa bila kuzingatiwa viwango vya lazima vya usalama. Amesema licha ya hayo nyumba hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na Waislamu kwa miaka mingi kwa lengo la kusimamisha swala za jamaa imekuwa ikiwakera baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanaodai kuhatarishwa maisha yao eti kutokana na mahudhurio ya Waislamu katika nyumba hiyo. Waislamu wamekasirishwa sana na hatua hiyo na kumtaka meya wa Nice kuwapa sehemu nyingine inayofaa kwa ajili ya kusimamaisha swala zao za jamaa. Wanasema wanaunda asilimia 10 ya wakazi wote wa mji huo na kwa hivyo wana haki ya kupewa sehemu ya kutekelezea ibada zao. 1025032
captcha