IQNA

Msikiti mkubwa zaidi wa Uturuki kujengwa katika mji wa Diyarbakir

18:24 - June 10, 2012
Habari ID: 2343720
Msikiti mkubwa zaidi nchini Uturuki unatarajiwa kujengwa katika mji wa Diyarbakir. Msikiti huo ambao utakuwa wa kisasa kabisa utafanana na ule wa Mtume (saw) mjini Madina na umepangwa kujengwa katika kiwanja kilicho na ukubwa wa mita mraba 51,000.
Wajenzi wa msikiti huo wanasema kuwa utakuwa na uwezo wa kubeba waumini 20,000 kwa wakati mmoja. Vilevile hatua zimechukuliwa kwa lengo la kuwawezesha walemavu na wasiojiweza kimwili kuingia kwenye msikiti huo wenyewe bila kusaidiwa na mtu yoyote na kunufaika na hotuba, mawaidha pamoja na huduma nyingine zinazotolewa msikitini humo. Kwa mfano vipofu wataweza kuingia kwenye msikiti huo bila msaada wa mtu wa pili ambapo watoongozwa kuingia humo na kuketi sehemu maalumu waliyotengewa kwa msaada wa sauti. Vilema pia wataweza kuingia msikitini humo moja kwa moja kwa kutumia viti vyao maalumu vinavyowasaidia kutembea. Visiwi pia watasaidiwa na wataalamu kuweza kunufaika na mafunzo, mawaidha na hutuba za Ijumaa zitakazotolewa msikitini humo. Hakuna msaada wowote wa kifedha utakaotoka kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo bali utajengwa kwa fedha zitakazotolewa na watu wanaojitolea. 1026819
captcha