Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Ukurubishaji wa Madhehebu ya Kiislamu, kongamno hilo la siku tatu ambalo litawashirikisha wasomi, wanazuoni na wanafikra mashuhuri wa Kiislamu wakiwemo Ayatullah Ali Taskhiri, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu na wanazuoni mashuhuri wa Pakistan limepangwa kufanyika katika miji ya Islamabad na Lahore. Ayatullah Taskhiri ataongoza ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kongamano hilo. 1026525